Course information

PPIZ inafuraha ya kutangaza kozi ya ngazi ya kimataifa ya PDC mnamo Mei 2023. Kozi hii inafuata muundo wa masaa 72 uliothibitishwa kimataifa ambayo itahusisha nyanja zote za Permaculture. Itajumuisha mada kama vile uzalishaji wa chakula, usimamizi wa rasilimali, usimamizi wa miradi, udongo, kilimo msitu, mifumo ya wanyama, teknolojia sahihi, mifumo ya maisha ya watu na namna ya kuunda mikakati wa kusimamia rasilimali kiujumla.  Vilevile kozi itajumuisha ujuzi wote wa msingi wa permaculture, maadili, kanuni na mbinu za kubuni ambazo zinaweza kutumika katika mazingira na hali ya hewa yoyote.